Wednesday, February 3, 2016

Mgeni wa Mke wangu(Mwanaume), anahudumiwa na mke wangu zaidi yangu


Habari zenu wanajamvi,

Naombei msaada katika hili, rafiki yangu ameoa na ana watoto wawili chini ya miaka mitano,majuzi mkewe kamkaribisha mwanaume mwenye mtoto toka kijijini kwao Kwediboma,Handeni ili aje hapa Tanga mjini kwa ajili ya matibabu ya mwanawe.

Jamaa anaishi nyumba ya vyumba viwili na sebule na huyo mgeni wa mke wake amepewa chumba chake,jamaa kinachomuumiza kichwa ni mwenendo wa mkewe kumuandalia maji ya kuoga na kumuhandle huyo mgeni wa kiume kwa heshima kubwa bila yeye mumewe kutowahi kupata huduma hizo siku za nyuma.

Ameshamwambia mkewe kuwa hamhitaji mgeni huyo nyumbani kwake,ila mkewe amejitetetea kuwa jamaa hana mwenyeji mwingine hapa mjini.

Kesho ni siku ya jamaa(mgeni wa huyo mwanamke) kwenda kliniki Bombo hospitali kwa ajili ya upasuaji wa henia ya mwanawe,na hapo ndipo dereva la daladala anapopata shaka zaidi ya kukosa kumuona mkewe kwa kuwa atakuwa bize kumpelekea chakula jamaa na mwanaye hospitalini.

Dereva wa daladala amechanganyikiwa,anaomba ushauri wenu afanye nini? Yaani mpaka mishipa ya kichwa imemtoka na anaonekana kukosa amani kabisa.


0 comments:

Post a Comment