Saturday, April 9, 2016

Mchumba wangu hatakiwi kwetu nifanyaje?


Habari zenu Wanajamvi,
Natumaini wote ni wazima wa afya njema,  Nia na madhumuni ya kuandika waraka huu ni kuomba ushauri kwani naamini penye wengi pana mengi......... Nina  mpenzi wa miaka minne  toka tuanze mahusiano yetu na kama ilivyo kawaida mkiwa kwenye mahusiano lazima muwe na mipango mingi ya maisha yenu ya kifamilia hapo baadae  hasa ndoa pamoja......

Kwa kuwa nampenda mpenzi wangu nikaona si vibaya kama nikienda nae nyumbani waanze kumzoea na yeye kuwafahamu ndugu zangu wengine.....

Sasa baada ya kumpeleka nyumbani siku  nikawekewa kikao cha familia na kuambiwa kuwa mtu nilienae hanifai, ana background mbaya na hawapo tayari kuona mimi nikimuoa huyo binti.....

Nilijitetea sana kumsafisha mpenzi wangu aonekane si mtu mbaya kama wanavyosema ila juhudi zangu ziligonga mwamba kabisa, na kuniambia hawamtani na nisiende nae tena nyumbani siku nyingine!!!1

Naomben ushauri, Mpenzi wangu bado napmpenda.......je nimwambie mpenzi wangu hali halisi ilivyo? Maana toka siku hiyo akiniambia habari za yeye walivyompokea nyumbani nafsi yangu inakuwa inanisuta

Uncle J Dar